WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye leo Januari 11. 2017 amemkabidhi bendera ya Taifa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika sherehe za ufunguzi wa michuano ya AFCON 2017 itakayofanyika nchini Gabon.
Makabidhiano hayo yamefanyika wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni waalikwa pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.
Post a Comment