Everton Yakubali Kutoa Pauni Milioni 22 Kumnasa Schneiderlin
KLABU ya Everton imekubali kutoa kitita cha pauni milioni 22 kumnasa kiungo wa kati wa Manchester United Morgan Schneiderlin.
Everton imekubali kutoa kitita hicho walichohitaji United hivyo Morgan ambaye ni raia wa Ufaransa atajiunga na klbau hiyo muda wowote
Morgan, 27, alinunuliwa na Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 25 kutoka Southampton mwezi Julai 2015 chini ya kocha wa wakati huo Louis van Gaal.
Kocha wa Man U, Jose Morinho amesema Naibu Mwenyekti Ed Woodward amemuarifu kwamba mpango wa kumuuza staa huyo unakaribia kukamilika.
Morgan ameiwakilisha Man U mara 47, japo chini ya ukufunzi wa Jose Morinho amecheza mara 8 pekee, mara tatu katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Post a Comment