0


WEKUNDU wa Msimbazi 'Simba SC' usiku huu wametinga fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kuwachapa watani wao wa jadi 'Yanga SC' kwa penalti 4-2 kwenye mechi ya nusu fainali iliyopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katika mtanange huo uliokuwa wa kukatana na shoka ulishuhudiwa dakika 90 zikimalizika kwa matokeo ya 0-0, huku kila timu ikicheza kwa tahadhari kubwa ili kulilinda lango lake.

Baada ya dakika 90 kumalizika kwa matokeo ya bila kufungana, mwamuzi wa mchezo aliamuru yapigwe matuta.

Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupiga penalti kupitia kwa nahodha wao Jonas Mkude na matokeo ya penalti yalikuwa hivi:

Waliofunga penalti kwa upande wa Simba ni Mkude, Agyei, Mzamiru na Bosungu huku Mwamjali akikosa penalti ya tatu na kuifanya timu yake kupata penalti 4 kati ya 5.

Yanga waliopata penalti ni Msuva, Kamusoko huku Mnishi na Mwinyi wakikosa penalti na kuipa Simba nafasi ya kutinga fainali.


Kwa matokeo ya leo, Simba atakutana na Azam FC katika fainali itakayochezwa Januari 13 saa 2:15 usiku.

Azam wametinga fainali baada ya kuifunga Taifa Jang'ombe bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo jioni.

Post a Comment

 
Top