Man U Waichapa 2-0 Hull City, Wanusa Fainali Kombe la EFL
VIJANA wa Jose Mourinho, Manchester United wameendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa Kombe la EFL baada ya jana usiku kuibuka kidedea kwa kuichapa Hull City mabao 2-0 kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Man U yaliwekwa kimiani na Juan Mata dakika ya 56 pamoja na Marouane Fellaini kwenye dakika ya 86.
Timu hizo zitarudiana tena Januari 26 mwaka huu ili kujua mshindi ni nani ambaye atacheza fainali Februari 26, 2017 na mshindi kati ya Liverpool na Southampton.
Post a Comment