0


OFISA Habari wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara amewamwagia sifa waamuzi wa mchezo wa jana wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi uliowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga ambapo Simba waliibuka kifua mbele kwa penalti 4-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa 0-0.

Akiongea kupitia Radio EFM katika Kipindi cha Sports HQ, Manara amesema alifurahishwa sana na waamuzi wa mchezo wa jana maana walizingatia vyema sheria 17 za soka na kuwataka waamuzi wengine kujifunza kutokana na waamuzi hao.

Mbali na pongezi hizo, Manara pia amewapongeza wachezaji wa Simba kwa ushindi huo uliowakatia tiketi ya kutinga fainali ambapo watakwaana na Azam Ijumaa ya Januari 13, 2017.

Post a Comment

 
Top