0






KLABU ya Arsenal ya jijini London imekamilisha usajili wa kinda mwenye miaka 20, aitwaye Cohen Bramall baada ya kufaulu majaribio ya kujiunga na timu hiyo.

Cohen ambaye ni beki wa kushoto, mwezi Desemba mwaka jana aliachishwa kazi katika kiwanda cha kutengeneza magari cha  Bentley Motors huko Crewe, England alipokuwa akijipatia riziki.


Hapo awali kinda huyo alifanya majaribio na klabu za Crystal Palace na Sheffield.


Arsenal kupitia katika tovuti yao wamethibitisha kumnasa kinda huyo ambaye ataongeza nguvu katika kikosi cha under 23 kabla ya kuwania namba kwenye kikosi cha wakubwa.
Kiwanda alipokuwa anafanya kazi Cohen.

Dogo huyo atakuwa akilamba £3,000 kwa wiki ambayo ni neema kwake maana kule kiwandani alikuwa akilipwa £400 kwa wiki.

Post a Comment

 
Top