MCHEZO wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, kati ya Azam FC na Taifa Jang'ombe umemalizika muda huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambapo Azam FC wameibuka kidedea kwa bao 1-0 na kutinga fainali ya michuano hiyo.
Bao hilo la pekee la Azam limefungwa na Frank Domayo katika dakika ya 33 ya kipindi cha kwanza baada ya kupiga shuti kali lililomuacha mlinda mlango wa Taifa Jang'ombe.
Kwa matokeo hayo, Azam FC wanamsubiri mshindi kati ya Simba na Yanga ili wakwaane naye katika fainali itakayopigwa Januari 13, 2017.
Post a Comment