0

Nahodha wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Steven Gerrard atarejea katika klabu hiyo kama kocha wa kikosi cha wachezaji chipukizi.

Gerrard mwenye umri wa miaka 36 ambaye alichezea Liverpool mechi 710 na kushinda vikombe tisa kuanzia mwaka 1998, ataanza kazi rasmi mwezi Februari.

Kiungo huyo wa kati aliondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2014-15 na kujiunga na klabu ya LA Galaxy inayocheza ligi kuu ya soka ya Marekani na Canada (MLS).

Alistaafu kuchezaji soka Novemba mwaka jana baada ya kucheza kwa miaka 19.

"Ni kama kukamilisha mduara, kurejea mahali ambapo yote yalianzia," Alisema Gerrard

Post a Comment

 
Top