0


Memphis Depay ametua katika klabu yake mpya ya Lyon baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United.

Depay amejiunga na Lyon kwa ada inayokadiriwa kufikia £16m ila huenda ikafikia £21.6m, ukiongeza na marupurupu yatakayotegemea miongoni mwa mengine iwapo Lyon watafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Depay kupata mkataba mpya.

United pia wameweka kifungu cha kuwawezesha kumnunua mchezaji huyo tena iwapo watamhitaji pamoja na kuwa na usemi kuhusu kuuzwa kwake.

Depay, 22, amefunga mabao saba katika mechi 53 alizocheza tangu kujiunga na United kwa £31m akitokea PSV Eindhoven Mei 2015.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Depay amewaaga mashabiki wa Man U na kuwashukuru akisema ushirikiano waliomuonyesha akiwa klabuni hapo kamwe hawezi kuusahau.

Post a Comment

 
Top