AFCON 2017: Morocco Yaichabanga 3-1 Togo
Kikosi cha Morocco usiku huu kimeibuka na ushindi mnono katika mechi yake kutoka Kundi C kwenye michuano ya AFCON 2017 baada ya kuichapa mabao 3-1 Togo.
Togo ndiyo waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Morocco katika dakika ya 5 ya mchezo kupitia kwa Mathieu Dossevi kisha Morocco kusawazisha bao hilo dakika ya 14 kupitia kwa Aziz Bouhaddouz.
Mabao mengine ya Morocco yalipatikana kupitia kwa Romain Saiss dakika ya 21 na Youssef En-Nesyri dakika ya 72 na kufanya matokeo kuwa 3-1 hadi mwisho wa mchezo.
Matokeo hayo yanazidi kulifanya Kundi C lenye timu za Ivory Coast, DR Congo, Morocco na Togo kuwa gumu maana hadi sasa hakuna timu yenye uhakika wa kuingia robo fainali baada ya kila timu kucheza michezo miwili na kubakiwa na mechi moja tu.
Kundi hilo linaongozwa na DR Congo wenye pointi 4, wakifuatiwa na Morocco pointi 3 kisha Ivory Coast wenye pointi 2 na Togo ikiwa mkiani na pointi 1.
Vikosi vilikuwa hivi;
Morocco XI: Munir, Benatia, Da Costa, Saïss, Dirar, El Ahmadi, Boussoufa, Mendyl, El Kaddouri, Bouhaddouz, Fajr
Togo XI: Agassa, Ouro-Akoriko, Djene, Dossevi, Romao, Atakora, Bebou, Atiye, Gakpe, Adebayor, Laba
Post a Comment