0







KIKOSI cha Antonio Conte, Chelsea jana kimezidi kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa bao 3-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Leicester City.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa King Power ambapo wenyeji walikuwa Leicester City, Chelsea walipata mabao yao kupitia kwa Marcos Alonso aliyefunga mawili na Pedro aliyetupia moja.

Kwa ushindi huo, Chelsea wamefikisha pointi 52 wakiwa nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo yenye jumla ya timu 20 baada ya kucheza mechi 21.

Post a Comment

 
Top