0







KIKOSI cha Washika Bunduki wa London, Arsenal jana kiliibuka na ushindi mnono wa bao 4-0 dhidi ya Swansea City katika mtanange wao wa Ligi Kuu ya England 'Premier League'.

Wafungaji katika mchezo huo walikuwa Olivier Giroud, Alexis Sanchez huku mabao mengine mawili wachezaji wa Swansea City Jack Cork na K.Naughton wakijifunga.

Katika mchezo huo, Alexis Sanchez aliibuka mchezaji bora wa mchezo.

Kwa matokeo hayo, Arsenal imefikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea na Tottenham Hotspur baada ya kucheza michezo 21.

Post a Comment

 
Top