0


Gabon wakishangilia bao lao lililofungwa na Aubameyang katika dakika ya 52.

Aubameyang akiifungia Gabon bao.

Guinea-Bissau wakishangilia baada ya kusawazisha bao dakika ya 90.

MWENYEJI wa michuano ya AFCON 2017, Gabon jana ameshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Guinea-Bissau kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo uliopigwa huko Libreville.

Gabon ndiyo walikuwa wa kwanza kujipatia bao lao kupitia kwa straika anayeichezea timu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang katika dakika ya 52.

Katika dakika ya 90 ya mchezo, Juary Soares alivuruga furaha ya wenyeji baada ya kuisawazishia timu yake ya Guinea-Bissau kwa mpira wa kichwa na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Mechi ya pili ilizikutanisha timu za Burkina Faso na Cameroon zote kutoka Kundi A ambazo nazo zilitoka sare ya bao 1-1 wafungaji wakiwa Benjamin Moukandjo wa Cameroon na Issoufou Dayo akiifungia Burkina Faso.

Kwa matokeo hayo, timu zote za Kundi A kila moja ina pointi 1.

Post a Comment

 
Top