0

KLABU BIngwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, usiku huu imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 31 na kubakia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 14 na kinara Simba mwenye pointi 45, ambayo nayo imelazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar jioni ya leo.

Azam FC iliuanza mchezo huo kwa kasi ikitka kupata bao la mapema, lakini safu ya ulinzi ya Mbeya City ilikuwa imara kuondoa hatari zote zilizokuwa zikifanywa na washambuliaji nahodha John Bocco na Yahaya Mohammed.

Post a Comment

 
Top