KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo kimeshindwa kuondoka na pointi 3 katika mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Wakata Miwa, Mtibwa Sugar baada ya kulazimishwa suluhu.
Katika mtanange huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro timu zote mbili zilionekana kupata tabu kutokana na ubovu wa uwanja na kuamua kucheza mchezo ambao haukuvutia sana kwa watazamaji kutokana na pasi nyingi kupotea uwanjani na kupigwa kwa mipira mirefu kila mara na kupelekea hadi mwisho wa mchezo matokeo kuwa 0-0.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 45 ikiendelea kukaa kileleni mwa ligi hiyo huku ikifuatiwa na mahasimu wao Yanga SC wenye pointi 43.
Post a Comment