Pierre-Emerick Aubameyang akiisawazishia Gabon kwa penalti. |
Burkina Faso wakishangilia bao lao lililofungwa na Nakoulma. |
Nakoulma (kulia) baada ya kuifungia Burkina Faso. |
Aubameyang (kushoto) baada ya kufunga penalti akishangia na mwenzake. |
MWENYEJI wa michuano ya Kombe la AFCON 2017, Gabon amezidi kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu kuingia hatua ya robo fainali baada ya leo usiku kulazimishwa sare nyingine ya bao 1-1 na timu ya Burkina Faso.
Katika mtanange huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Burkina Faso ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya wachezaji wa Gabon kwenda kushambulia na wapinzani wao kupiga mpira wa 'counter-attack' uliomshinda beki wa Gabon, Obiang kuuzuia na kuchukuliwa na Nakoulma aliyewazidi ujanja na msuli mabeki na kuiandikia timu yake bao la kwanza dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza.
Gabon nao walikuja juu na kufanikiwa kupata penalti dakika ya 38 ya mchezo baada ya mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang kuangushwa na kipa wa Burkina Faso, Herve Koffi aliyezawadiwa kadi ya njano na kisha Aubameyang mwenyewe kupiga penalti hiyo na kuisawazishia timu yake.
Kwa matokeo ya leo, bado hali si nzuri kwa wenyeji hao wenye pointi 2 sawa na Burkina Faso katika Kundi A wakisubiri wenzao Cameroon na Guinea-Bissau wanaocheza usiku huu ambao nao kabla ya mechi hii wana pointi mojamoja kila mmoja.
Post a Comment