Hatua ya makundi ya michuano ya AFCON 2017 leo ndiyo inafika kikomo kwa mechi mbili za mwisho zitakazopigwa muda mmoja huko nchini Gabon kutoka Kundi D.
Misri watakipiga na Ghana ambao tayari wamekata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali huku Uganda ambao tayari wametupwa nje ya michuano wakipepetana na Mali.
Mpaka sasa, Ghana ndiyo wanaongoza Kundi D wakiwa na pointi 6 baada ya kucheza mechi 2 wakifuatiwa na Misri wenye pointi 4 nao wakiwa wamecheza mechi 2.
Mali na Uganda ndiyo wanaonekana kusuasua katika kundi hilo ambapo Mali ana pointi 1 baada ya mechi 2 huku Uganda kutoka Afrika Mashariki wakiwa hawana pointi yoyote baada ya kupoteza michezo yote miwili.
Post a Comment