Michuano ya AFCON 2017 leo inaingia siku ya pili baada ya kufunguliwa rasmi jana nchini Gabon.
Mechi za leo ni za kundi B lenye timu za Algeria, Zimbabwe, Tunisia na Senegal.
Katika mechi ya kwanza itakayopigwa saa 1:00 usiku huko Franceville, Algeria atakwaana na Zimbabwe kisha Tunisia na Senegal nao watajitupa uwanjani saa 4:00 usiku kwenye mchezo wa pili utakaochezwa hukohuko Franceville, Gabon.
Baada ya mechi za jana za ufunguzi zote kumalizika kwa sare ya 1-1, timu zote za Kundi A ambazo ni Gabon, Guinea-Bissau, Burkina Faso na Cameroon zote zina pointi mojamoja.
Post a Comment