Barcelona imezidi kukaribia taji la La Liga baada
ya kuifumua Almeria 4-0 katika mchezo ulioisha hivi punde.
Mshambuliaji Luis Suarez ambaye sasa ‘injini’ yake
inaanza kuchanganya vilivyo, akafunga mara mbili katika dakika ya 55 na
90.
Lionel Messi naye
hakubaki nyuma, alifunga bao moja kwenye dakika ya 33 huku beki Marc Bartra
akifunga katika dakika ya 75.
Barcelona (4-3-3): Bravo; Alves, Bartra, Mascherano, Adriano; Sergi Roberto,
Xavi, Rakitic; Messi, Suarez, Pedro.
Subs: Ter Stegen, Montoya, Mathieu, Pique, Iniesta,
Rafinha, Neymar
Almeria (4-2-3-1): Julian; Ximo Navarro, Marin, Trujillo, Casado; Partey,
Corona; Wellington Silva (Soriano), Espinosa (Mane), Edgar (Zongo); Bifouma.
Post a Comment