Mshambuliaji wa Kibrazil Philippe Coutinho
ameipeleka Liverpool nusu fainali ya FA Cup baada ya kuifungia bao pekee dhidi
ya Blackburn Rovers.
Huu ulikuwa mchezo wa marudiano baada ya mchezo wao
kwanza uliochezwa Anfield mwezi uliopita kumalizika kwa sare ya 0-0.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ewood Park,
Blackburn walibana hadi dakika ya 70 na kujikuta wakiruhusu bao lililowatupa
nje ya michuano.
Coutinho aligongeana pasi kadhaa na Jordan
Henderson pembeni mwa uwanja kabla hajaachia mkwaju wa chinichini uliompita
kipa Simon Eastwood.
Liverpool itamenyana na Aston Villa katika nusu
fainali itakayochezwa Wembley Jumapili ya
April 19.
Blackburn: Eastwood, Henley, Baptiste, Kilgallon, Olsson, Evans, Williamson,
Conway (Gestede 65), Cairney, Marshall, Rhodes.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Lovren, Sakho (Toure 28), Moreno, Henderson, Lucas,
Allen, Sterling, Sturridge (Lambert 85), Coutinho.
Post a Comment