Viongozi wa Azam wakilumbana.
Waandishi Wetu,Dar es SalaamHALI ya sintofahamu imetokea ndani ya Klabu ya Azam ambapo viongozi kadhaa wa timu hiyo juzi walivurugana hadharani na kutaka kutwangana makonde baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City, kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Tafrani hiyo ilitokea baina ya Meneja wa Azam FC, Jemedali Said na Mkurugenzi wa Ufundi wa Azam FC, Saady Kawemba ambapo walitaka kupigana baada ya kutokea mabishano makali kati yao.
Tukio hilo lilitokea ghafla baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ambapo inadaiwa walianza kuzozana juu ya matokeo na kubishana juu ya safari ya timu hiyo kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar.
Championi Ijumaa lilishuhudia wasamaria wema wakijaribu kuwatenganisha viongozi hao baada ya kuona hali mbaya huku wakiendelea kurushiana maneno.
Walipoulizwa suala hilo jana, Kawemba alisema alitoa maagizo lakini hayakufanyiwa kazi hivyo akaagiza mtu mwingine ayatekeleze, kuhusu kukwaruzana, alisema hayo ni mambo ya ndani ya klabu. Upande wa Jemedali alisema: “Ni jambo la kawaida kupishana katrika kazi lakini kila kitu kipo sawa.”
Post a Comment