MACHO na masikio ya wapenda burudani wote yamehamia
ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem,
jijini Dar ambapo wafalme wawili wa muziki Bongo, Mfalme wa Vigodoro,
Msaga Sumu pamoja na Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Kiba wataungana na
Malkia wa Masauti, Isha Mashauzi katika kuandika historia kwa mara ya
kwanza.
Akizungumza na Showbiz, mratibu wa burudani wa ukumbi huo, Abdallah
Mrisho ‘Abby Cool’ alisema kwamba hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa
wakali hao kukutana jukwaa moja la Dar Live na kuwaahidi kila mmoja kuwa
wa kitofauti katika kutoa burudani.
Ali Kiba
Kuhusiana na Mfalme wa Bongo Fleva, Abby alisema kuwa ni
muda mrefu kwa Ali Kiba kufanya shoo ndani ya uwanja huo kwani tangu
mwaka 2013 hajafanya shoo hapo hivyo mashabiki wa Ali Kiba na muziki wa
Bongo Fleva kwa pamoja wajiandae kwa sapraizi kibao kutoka kwake.
“Ali Kiba atashuka jukwaani kivingine na safari hii atashuka kama
Mwana Dar Live kutokana na wimbo wake unaotikisa kila kona wa Mwana,
mashabiki pia watapata burudani ya aina yake kwa kupigiwa nyimbo zote
kali za Ali Kiba kama vile Kimasomaso na huu ambao ni habari ya mjini
kwa sasa wa Chekecha Cheketua huku atakayecheza vizuri wimbo huo
tutamzawadia,” alisema Abby.
Msaga Sumu
Miongoni mwa wafalme watakaosumbua siku hiyo ni Msaga
Sumu ambaye amekuwa hana mpinzani katika muziki wa vigodoro.“Wakazi wote
wa Temeke na jiji zima la Dar hii si ya kukosa kwani Msaga Sumu
atawaunganisha pamoja waswazi na wakishua katika kuwapa ngoma zake zote
kali kama vile Hunifai, Apangalo Mola pamoja na Marafiki Gani.“Kwa mara
ya kwanza ndani ya Dar Live, Msaga Sumu atazindua wimbo wake mpya kabisa
wa Kidole Changu,” alisema Abby.
Isha Mashauzi
“Zipo nyimbo nyingi zitakazosumbua siku hiyo, kama
tumjuavyo Isha akiwa stejini ni ‘Jike la Simba’ sasa pata picha akiwa na
bendi yake ya Mashauzi Classic wakidondosha wimbo baada ya wimbo.
“Miongoni
mwa nyimbo zitakazosumbua siku hiyo ni Ropokeni Yanawahusu, Ni Mapenzi
tu, Tupendane, Bonge la Bwana na huu mpya atakaouzindua kwa mara ya
kwanza ukumbini hapo wa Nimpe Nani.”
Masai Warriors
Mapema kuanzia asubuhi kundi la sarakasi la Masai
Warriors litakuwepo kwa ajili ya kutoa burudani kwa watoto na wote
watakaofika siku hiyo.Baada ya kutikisa kwenye Usiku wa Wafalme, Desemba
mwaka jana, Masai Warriors wamekuja upya na safari hii ni ya kipekee
kwa watoto wote kwani watawaburudisha kwa michezo kama vile yoga,
vichekesho, kuvuta kamba, kucheza na gunia na mingine mingi.
Watoto pia watapata burudani ya kipekee kwa kuogelea, kubembea, kuteleza na kupanda ndege ‘spesho’ iliyopo ndani ya Dar Live.
Wadhamini
Vodacom
Burudani zote hizo zimeletwa kwenu kwa
udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ambayo mtandao wake
umeenea nchi nzima na viwango vyake ni bei nafuu.
Valeur
Kinywaji murua kinachopendwa na wengi ambacho kwa sasa
kinapatikana kote Tanzania kwenye ‘viroba’ na katika chupa. Chupa yake
ipo katika muonekano mpya kabisa wa kimataifa.
Redbull
Kinywaji kinachokupa nguvu zaidi na kukuondoa katika uchovu. Redbull
pia wamekuja na vinywaji murua vingine kama vile Skyy, Jagermiester,
Grants vyenye ladha ya kipekee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment