BAADA ya kuiongoza vyema timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Mgambo JKT, winga Simon Msuva amewataka mashabiki wa
klabu hiyo wasubiri sherehe za ubingwa Jangwani.
Yanga waliutafuna mfupa ulioishinda Simba baada ya kuifunga Mgambo,
juzi. Mgambo waliiaibisha Simba baada ya kuwafunga wekundu hao wa
Msimbazi mabao 2-0, Jumatano iliyopita.Katika ushindi wa Yanga juzi,
Msuva aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 77, kabla ya Amissi
Tambwe kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 83.
“Ninashukuru sana kushinda mchezo huu, maana nilikuwa nikiuwaza
kutokana na ugumu tunaokutana nao tukiwa katika uwanja huu, kupata
pointi tatu ni kitu cha kujivunia kwetu.
“Tunachoangalia kwa sasa ni ubingwa na unaonekana upo karibu ingawa
upinzani ni mkubwa sana, kinachotakiwa ni ushirikiano kuanzia kwa
wachezaji mpaka mashabiki ili kufanikisha hilo kwa nguvu ya pamoja,”
alisema Msuva ambaye sasa amefikisha mabao tisa kwenye Ligi Kuu Bara,
akimfukuzia Mrundi, Didier Kavumbagu kwa tofauti ya bao moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment