Simba vs Yanga, Mtoto Hatumwi Sokoni Leo
HATIMAYE siku iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki wa soka hapa nchini leo imetimia ambapo miamba miwili ya soka Simba SC na Yanga SC itakapokuwa ikikwaana katika mpambano wa kusaka tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Mtanange huo wa nusu fainali utapigwa saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Timu itakayoibuka kidedea katika mpambano wa leo itakutana katika fainali itakayochezwa Januari 13 na mshindi wa nusu fainali ya kwanza itakayopigwa hapo baadaye kidogo saa 10:15 jioni kati ya Azam FC na Taifa Jang’ombe.
Mpaka muda huu mashabiki wa watani hao wa jadi bado hakuna upande wenye uhakika wa kuibuka kifua mbele mbali na Yanga kupokea kichapo kikali kutoka kwa Azam FC katika mechi yao ya mwisho ya Kundi B wakati Mnyama akimaliza mechi yake ya Kundi A kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys.
Kitakachomaliza ubishi ni dakika 90 za mpambano huo.
Post a Comment