0



KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba amewaambia mashabiki wa timu yake kwamba hataacha kupambana kwa ajili ya timu.


Pogba ameyeleza hayo katika ujumbe aliouandika kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya mtanange wao dhidi ya Liverpool jana uliomalizika kwa sare ya 1-1 huku staa huyo akisababisha penalti baada ya kuunawa mpira wakati akiruka kichwa kuuokoa.

Pogba ameandika hivi; "Hiyo utokea pale tunapohitaji kuwa na nguvu. Nipo hapa, tayari kupambana na nipo tayari kwa mechi nyingine!! Napenda kuwashukuru mashabiki ambao kila wakati wapo pamoja na mimi na wanaendelea kuniamini. Angalau hatukupoteza mchezo. Sitaacha kupambana!"

Post a Comment

 
Top