0


Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil amerejea kikosini baada ya kuwa nje kutokana na kuugua.

Ozil atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoikabili Swansea City hapo kaesho katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya England.

Wakati huo, bosi wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger amesema hana wasiwasi wowote kuhusu suala la mkataba wa staa wake huyo aliyerejea kikosi maana bado kuna muda katika mkataba wake wa sasa.
Wenger.

Mwanzoni mwa wiki hii, Ozil alinukuliwa akisema kuwa mkataba wake wa kuendelea kuitumikia Arsenal utategemeana na kocha wake huyo.

Kiungo huyo amebakiza miezi 18 katika mkataba wake wa kuichezea Arsenal lakini Wenger hana wasiwasi mbali na staa huyo kutaka mshahara ambao ni mkubwa kuliko kiwango cha mishahara ya klabu hiyo.

Mastaa wengine ambao wamerejea kikosini na wako fiti kuwavaa Swansea kesho ni pamoja na Laurent Koscielny, Petr Cech na Alexis Sanchez.

Post a Comment

 
Top