0


MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa, ameonyesha kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo wakati wowote, aliposema kuwa analichukia soka la England.

Kocha wa timu hiyo Antonio Conte, alimuondoa mshambuliaji huyo kwenye kikosi chake kilichovaana na Leicester City wikiendi iliyopita kwa kile kilichodaiwa kuwa alikorofishana na mmoja kati ya makocha wa timu hiyo.

Costa, 28, yupo kwenye mkata­ba na timu hiyo hadi mwaka 2019 na Chelsea waligoma kumuuza kwenye usajili wa majira ya joto yaliyopita, lakini sasa inaonekana kuwa anaweza kuondoka.

Taarifa zinasema kuwa Conte atakuwa na kikao na mchezaji huyo kesho kujadili kuhusu sakata hilo.

“Diego alifanya mazoezi Jumanne na kusikia maumivu kwenye nyama za miguu, haku­fanya mazoezi tena na kwa sababu hiyo akakosekana kwenye mchezo uliopita,” alisema kocha huyo.

Gazeti la SunSport limeripoti kuwa linajua mchezaji huyo aliko­rofishana na kocha wa viungo mazoezini na wakala wake amekuwa akipambana sasa kuhakikisha kuwa anamtafutia timu nchini China.

Inaelezwa kuwa aliwaambia wenzake kuwa atafanya kila linalowezekana ili aondoke kwenye timu hiyo kwa kuwa analichukia soka la England pamoja na Chama cha Soka England (FA).

Chanzo kutoka nchini China kimesema: “Costa ni chaguo la kwanza hapa, tunajua kuwa anataka kuja kucheza huku.”

Post a Comment

 
Top