0

Kikosi cha Azam FC usiku huu kimefanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya tatu baada ya kuichapa Simba SC bao 1-0.

Alikuwa ni Himid Mao katika dakika ya 13 ya mchezo aliyeipatia Azam FC bao pekee na la ushindi akipiga shuti kali lililomuacha mlinda mlango wa Simba Agyei na kuifanya timu yake kuweka rekodi ya kutwaa kombe hilo bila kufungwa bao lolote.

Aidha baada ya mechi, jopo la makocha limemchagua beki wa Azam FC, Aggrey Morris, kuwa mchezaji bora wa fainali.

Kwa ushindi wa leo, Azam watakuwa sawa na Simba wote wakilitwaa kombe hilo mara tatu kila mmoja.

Post a Comment

 
Top