Arsenal inafanya juu chini kuhakikisha inamsajili supastaa wa klabu ya FC Porto ya Ureno, Yacine Brahimi (pichani kulia) katika usajili ujao wa kiangazi.
Raia huyo wa Algeria ameibuka kuwa mmoja wa wachezaji bora nchini Ureno baada ya kuanza kwa kishindo katika timu hiyo akitokea Granada.
Brahimi ndiye kiungo anayeongoza kwa mabao katika Champions League msimu huu, huku Manchester United na AC Milan zikihusishwa kumuwania.
Porto haiko tayari kumuuza kwa bei ya kutupa, na inaaminika Arsenal ina uwezo wa kulipa dau la pauni milioni 33 kuweza kumaliza biashara.
Post a Comment