0
Timu ya Bayern Munich ya Ujerumani na Paris St. Germain ya Ufaransa zimesonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya kufuatia matokeo waliyayapata usiku wa kuamkia leo.


Wakicheza kwa kujiamini Bayern Munich ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali katika mashandano hayo baada ya baada ya kuwapa kichapo cha mbwa mwizi wapinzani wao Shakhtar Donetsk ya Ukrine cha magoli 7- kwa mtungi.
Magoli ya Bayern Munich yalitiwa kimiani na Thomas Muller, Jerome Boateng ,Franck Ribery,Holger Bastuber, Robert Lewandowski na Mario Gotze.
Nayo Paris St. Germain ya Ufaransa imesonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kuwaondoa Chelsea katika mashindano hayo japo timu hizo zilitoka sare ya magoli mawili kwa miwili lakini magoli ya ugenini iliyoyafunga hapo jana ndio yaliyowanufaisha Paris St. Germain.
Hivyo mshindi katika mechi hiyo ilibidi kupatikana katika dakika thelathini za nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida kumalizika huku timu zote zikiwa zimefungana goli moja kwa moja.
Wakiwa na matumaini ya kuingia robo fainali Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia Gary Cahill katika 81 lakini Mlinzi wa zamani wa Chelsea David Luiz akafutilia ndoto hizo mbali baada ya kusawazisha goli hilo katika dakika ya 86.
Na hivyo hadi dakika 90 za kwanza zinamalizika Chelsea 1 na Paris St. Germain 1 na hivyo kulazimika kucheza dakika 30 nyingine ili kumpata mshindi.
Hata hivyo siku ya kufa nyani miti yote huteleza kwani mbali na Chelsea tena kuwa wa kwanza kupata goli kwa njia ya penalti kupitia kwa Eden Hazard katika dakika 96 na kufufua matumaini ya kusonga mbele, ndoto hizo tena zilifutiliwa mbali pale mlinzi mwingine wa Paris St. Germain Thiago Silva alipopachika goli liliisukumia moja kwa moja Chelsea nje ya mashindano hayo.

Post a Comment

 
Top