BAO la dakika za lala salama la
Willian, limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton usiku huu katika mcheo
wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Everton walifungwa bao hilo
baada ya kumpoteza mchezaji wake, Gareth Barry aliyetolewa kwa kadi nyekundu na
sasa The Blues wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi.
Steven Naismith alikuwa mwenye
bahati baada ya kuepuka adhabu licha ya kuunawa mpira kwenye boksi la Everton
kipindi cha kwanza.
Post a Comment